MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Utalii na Mahoteli

ngawaje Tanzania katika kipindi cha Nyerere haikuwa wazi katika kulizumgumzia suala la faida ya utalii (katika uchumi) serikali ilimiliki majengo kadhaa. Ilijenga mahoteli na loji kama vile loji ya Mafia iliyoanzishwa miaka ya 1960 badala ya klabu ya zamani ya uvuvi, iliyokuwa inavutia wavuvi wengi kutokea nje kwa miaka mingi. Loji hii imebinafsishwa kwa sasa na kuna mipango ya kuitanua zaidi.

Hivi karibuni hoteli mbili zimejengwa katika maeneo hayo ya Utende:

Ya tatu iko kisiwani Chole jirani na maeneo ya utende:

Harbour View hotel in Kilindoni Hoteli zote hizi zinamilikiwa na kuendeshwa na wageni. Vilevile kuna hoteli ndogondogo zinazomilikiwa na wazawa ambazo hutoa huduma kwa watanzania (kama vile watumishi wa serikali na mara nyengine kwa wageni wasiomudu gharama za hoteli kubwa). Hoteli hizi ndogondogo ni kama vile New Lizu mjini Kilindoni, Harbour View inayopakana na bandari ya Kilindoni, na Sunset View iliyopo Kilimani kisiwani Chole (email: kilimani04@hotmail.com).

Wakati utalii unaweza kuwa ni suluhisho la umaskini na kukosa maendeleo, vilevile utalii unaweza kuleta madhara kadhaa:

    Ground of Kilimani Hotel
  • Kupoteza haki za kumiliki ardhi sehemu za pwani kwa wenyeji
  • Kupigania rasilimali kama vile maji
  • Tabia na tamaduni za baadhi ya wageni ambazo haziendani na maadili ya wenyeji kama vile kwenda uchi au kuchukua picha za wenyeji bila ridhaa yao

Mahitaji ya watalii kwa karibu yote yanatoka nje ya eneo la Mafia (na pengine nje ya nchi), hali hii inasababisha kutokuwepo kwa soko labidhaa za wenyeji. Ikiwa matumizi ya nguvu kazi ya wenyeji isipokuwa kwenye maeneo duni na yasiohitaji ujuzi mkubwa kama vile bustani na ulinzi hivyo kuchangia kiasi kidogo tu kwa uchumi wa wenyeji.

Coconut tree marked with hotel developer's initials Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na mwamko wa utalii unaozingatia uhifadhi wa mazingira hivyo kujali maisha ya wenyeji na maeneo hayo yanazunguka sehemu hiyo ya utalii: (angalia kwa mfano Tourism Concern's website on (www.tourismconcern.org.uk).

Sera ya serikali ya Tanzania ni kuendeleza maeneo ya kusini kwa kuzingatia utalii-mazingira kama ilivyobainishwa na Waziri wa Utalii Mheshimiwa Meghji katika taarifa yake ihusuyo 'Statement on eco-tourism' iliyonukuliwa katika Swahili Coast magazine).

Makampuni kadhaaa yanayojihusisha na utangazi wa biashara ya utalii wa Kisiwa cha Mafia wamedai kuwa maeneo ya vivutio vya utalii vya Mafia vinazingatia uhifadhi wa mazingira na vinachangia kuongeza pato la uchumi wa wenyeji. Hivyo kuwalenga wale watalii na wageni wenye mitazamo ya kijamii katika mitandao kama vile www.responsibletravel.com. Si hoteli zote zinajihusisha na utoaji wa huduma za jamii inayoizunguka, ni hoteli ya Chole pekee iliyo mfano wa kuigwa kwani imejiwekea mikakati ya kuinua hali za wananchi katika maeneo yanayoizunguka hususan miradi ya maendeleo. Haya yameelezwa waziwazi katika makala ya mojawapo ya mmiliki wa hoteli hiyo aitwaye Jean de Villiers, katika makala yake yaitwayo 'Projects on Chole Island: Chole Mjini Conservation and Development Company Ltd' yanayopatikana katika www.africatravelresource.com/africa/E/tanzania/accommodation/s/TO2-mafia/03.TCHO/TCHOS.doc

Hatahivyo baadhi ya wakala wa utalii hujenga picha ya kisiwa cha Mafia kuwa ni kisiwa cha utulivu, 'pepo', isiyojulikana na iliyonyuma kimaendeleo kwa kiasi cha miaka 30 au zaidi ya kisiwa cha Zanziba. Ni kisiwa kinachoonekana kuwa nyuma, ambacho hakijachafuliwa wala kuathirika na maendeleo ya duniani. Kwa upande mkubwa wa maelezo yao ya 'kikuuza' kisiwa hicho kwa watalii, wao hulenga kwenye fukwe na vivutio vya baharini kama vile uzamiaji, aghalabu kuwepo kwa maelezo yahusuyo wenyeji ambao kwa kifupi huelezewa kuwa ni washika mila (ikiwa na maana ni wacheshi, wavumilivu na wenye ukaribisho). Mojawapo ya tovuti imethubutu hata kutumia maelezo ya kisiwa cha Mafia ya mwaka 1896 ya mwanajiografia wa Kijerumani kuelezea maisha yalivyo hivi sasa kisiwani hapo kama vile hakuna mabadilko yoyote yaliojitokeza hadi sasa www.Mafiaisland.com/history/people1.htm.

Maelezo kama hayo mara nyingi hayaonyeshi picha halisi ilivyo. Kisiwa cha Mafia hakikujitenga na mabadiliko ya kihistoria bali kimekuwa ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo kwa kiasi cha miaka elfu moja sasa. Watu wake hawajajitenga na sewamekuwa ni sehemu muhimu nyingine za dunia bali wamekuwa washiriki katika utandawazi kama inavyoonyeshwa katika kurasa zilizomo katika tovuti hii na nyinginezo. Haiyumkini, mawakala wa utalii wenyewe wameligundua hilo hivyo wamehakikisha kuwa watalii wanapewa picha ya utulivu wa kisiwa cha Mafia, nakwamba ukaribu wake na Zanziba ambako hivi karibuni kulikosa utulivu hauathiri amani kisiwani hapo. Kwa upande mwengine wanatahadharishwa kuwa ingwa wakazi wa kisiwa cha Mafia ni waisilamu lakini sio wale 'wenye misimamo mikali' www.utalii.com/Mafia_Island/Mafia_Island.htm au machafuko ya kisiasa ya Zanziba hayana athari kisiwani www.africatravelresource.com/africa/E/tanzania/safariguide/T02-Mafia.htm.

Marejeo ya msingi na yale ya ziada yahusuyo utalii:

  • Burns, Peter, 1999. An Introduction to Tourism and Anthropology. London and New York: Routledge.

  • Crick, Malcolm. 1989. 'Representations of International Tourism in the Social Sciences: sun, sex, sights, savings and servility' Annual Review of Anthropology, 18:307-44.

  • Lea, John, 1988. Tourism and Development in the Third World. London and New York: Routledge.

  • MacCannell, Dean, 1992. Empty Meeting Grounds; The Tourist Papers London: Routledge

  • Selwyn, Tom, 1994. 'The Anthropology of Tourism: reflections on the state of the art' in A.S. Seaton et al. Tourism: the State of the Art. London: Wiley.