MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Idadi ya Watu wa Mafia na Asili zao

Kama inavyotarajiwa kutokana na historia yake ya kutatanisha, wenyeji wa Kisiwa cha Mafia wana asili ya mseto. Wengi hujiita Wambwera ama Washirazi na hudai kuwa wao ni wenyeji wa asili wa kisiwani hapo. Wamesambaa kisiwani pote haswa upande wa kaskazini ambako pia kuna wanaojiita Wapokomo. Upande wa kusini kuna kundi la watu ambao walikuwa watumwa kutoka bara waliotumika kama watumishi wasiolipwa katika mashamba makubwa. Vilevile kuna makundi mbalimbali ya watu wenye asili ya makabila ya jirani, Wapokomo na Washirazi. Kipo kikundi kidogo cha wanaodai kuwa na asili ya uarabu, wafanyabishara wachache wa kiHindi na kikundi kidogo cha Wazungu wanaojihusisha na miradi ya maendeleo na huduma za utalii. Uasili wa wenyeji hubadilika badilika sio kwa sababu ya kuhamahama, bali nikutokana na mabadiliko ya mazingira ya kihistoria. Leo unakuta wenyeji wenye asili ya kiAfrika wanajiita kwa kifupi Waswahili au Watanzania tu.

Lugha inayotumika kisiwani hapo na Tanzania kwa ujumla ni Kiswahili. Lakini Kisiwa cha Mafia kina lahaja yake ya KiNgome ambayo kwa sasa kinazungumzwa kaskazini na kimetafitiwa na mwanaisimu wa Kitanzania Ahmad Kipacha (2004). Wakazi wengi ni wa madhehebu ya kiIslamu ya Suni, lakini kuna Wakristo wachache (Wakatoliki, Waluteri, na Wapentekoste - tazama www.bethanybrookline.org/tanzania.asp and www.allover.viamission.org/projects/ice.html) wakiwemo watumishi wa serikali waliopangiwa kisiwani hapo. Wengi wapo katika makao ya wilaya ya Kilindoni lakini vilevile kuna makanisa katika vijii vichache.

Sensa ya idadi ya watu na nyumba ya 2002 inaonyesha kwamba Kisiwa cha Mafia kina wakazi zaidi kidogo ya 40,000.Angalia http://allover.viamission.org/projects/ice.html) http://www.tanzania.go.tz/census/districts/mafia.htm

Hii inaonyesha ongezeko la idadi ya watu tangia sensa ya mwisho ya 1988 ambapo idadi ya watu ilikuwa ni kiasi cha 33,000 tu. Idadi ya watu ilipungua katika kipindi cha karne ya 20 wakati wa utawala wa Wajerumani lakini iliongezeka maradufu kipindi cha utawala wa Waingereza kama jedwali linavyoonyesha:

Idadi ya Watu, Kisiwani Mafia kuanzia mwanzoni mwa karne ya 20 hadi 1988

  • 1910 - 14,450
  • 1911 - 11,950
  • 1912 - 11,514
  • 1919 - 9,795
  • 1924 - 8466
  • 1957 - 12,199
  • 1967 - 16,748
  • 1978 - 23,104
  • 1988 - 33,056
  • 2002 - 40,557
Kwa habari zaidi, bonyeza hapa (pdf file 84k) pdf