MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Vyama Hiari (NGO)

Taasisi mbalimbali za misaada zimekuwa zikisaidia miradi mbalimbali Kisiwani Mafia. Taasisi hizi ni kama vile NORAD (Chama cha Misaada cha Norway) na DFID (Department for International Development UK - Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza). World Wildlife Fund (WWF - www.panda.org) zimekuwa zikitoa msaada mkubwa kwa Hifadhi ya Bahari ya Mafia tangu 1991. Vilevile vyama vyenginevyo vya hiari bado vinasaidia ufadhili, mafunzo, au aina nyengineyo kama vile:

 • UNICEF imesaidia kuboresha afya za watoto: www.unicef.org
 • Chama cha Kinamama cha Norway kiitwacho Kvinnefronten kinatoa msaada kwa Chama cha Maendeleo ya Wanawake wa Chole, Mafia. Angalia (www.kvinnefronten-no/arkiv/andre.sprak/english).
 • Medicos del Mundo (Madaktari wa Dunia - chama cha Kispanishi) kinasaidia chama hiari cha MICAS (Chama cha kuzuia ukimwi na mgonjwa ya znaa Mafia) www.medicosdelmundo.org
 • CARE kimetoa misaada kwa vyama mbalimbali vya Hiari vikiwemo Kimama (chama cha kinamama), CHAMAMA (Chama cha Maendeleo cha Kisiwa cha Mafia) na MICAS angalia www.care.org
 • Born Free kimesaidia uhifadhi wa kasa na nguvu (www.bornfree.org)

Kisiwa cha Mafia kina yama hiari kadhaa. Kwa upande wa makao ya wilaya viko vyama vifuatavyo:

 • Kiwanga outside MICAS officeCHAMAMA (Changia cha Maendeleo ya Mafia - ni chama kinachojishughulisha katika masuala ya mazingira, miradi ya kujikimu, elimu ya UKIMWI. Hivi karibuni walipata msaada kutoka CARE kwa ajili ya kampeni dhidi ya maambukizo ya UKIMWI (tazama juu).
 • MICAS (Mapambano dhidi ya UKIMWI na magonjwa ya zinaa kisiwa cha Mafia) inashirikiana na Medicos del Mundo, na kwa sasa inajishughulisha na mpango wa udhibiti unaowalenga vijana ambao hawapo sekondari. Wanao watendaji wa kujitolea wanaojishughulisha na vijana waliopo mashuleni na nje ya shule (angalia juu).
 • Kimama - umoja wa kinamama
 • Tasisi ya Dini - muungano wa vikundi mbalimbali vya kidini vikijumuisha wakristo na waislamu.

Group of women at a CSWD members' meetingKwa upande wa kisiwa cha Chole: kuna vyama hiari vitatu vya wenyeji.

 • The Chole Social Development Society (CSDS)
 • The Chole Economic Development Society (CEDS)
 • The Chole Society for Women's Development (CSWD)

Vyama viwili vya mwanzo vinapokea mapato yake kutoka katika kodi wanyotozwa wageni wakaao katika Hoteli ya Chole Mjini (angalia sehemu ya utalii), Chama cha CSWD hufadhiliwa na vyama vya Wanawake wa Norway vya Kvinnefronten na Fokus (www.fokuskvinne.no/English).