MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Matatizo na huduma ya afya

Matatizo mengi ya afya husababishwa na umasikini:

Medical facilities on Mafia

Dr. Amos at the lab bench Kila kijiji kina zahanati na wahudumu kama vile madaktari, wakunga na manesi. Dawa zinagawanywa kila mwezi na gharama zake huchangiwa na serikali na wafadhili (m.f UNICEF). Matibabu na madawa ni bure na watoto wote hupewa chanjo ya polio, surua, kifua kikuu na chanjo ya DPT. Kuna kliniki ya watoto wadogo inayoangalia uzito na ukuaji wa watoto.

Kuna hospitali ya umma mjini Kilindoni ambayo imekarabatiwa hivi karibuni kutokana na ufadhili wa nje. Wagonjwa wanalazimika kulipia gharama za madawa na matibabu yaliyo gharama kubwa kwa walio wengi. (Tazama picha za hospitali http://www.remotemedicine.org/PLKilindoni.htm.

Kilindoni hospital - a newly refurbished wardReception at Kili hospital