MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Ikolojia pamoja na Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa Cha Mafia

Mafia Island Marine Park noticeboardMafia ni kisiwa kikubwa kilichopo pwani ya kusini ya Tanzania karibu na Bonde la Mto wa Rufijia. Kina urefu wa maili 30 kutokea kusini hadi kaskazini na upana wa maili kumi. Ukubwa wa Mafia ni sawa na nusu ya kisiwa cha Unguja ambapo ni kwa upande wa kaskazini. Kama kilivyo kisiwa cha Unguja ni kipande cha ardhi kilichoinuka kwa juu na sio kisiwa cha mafumbawe. Udongo wa Mafia kwa kiasi kikubwa ni mchanga na mandharii ni tambarare. Sehemu kubwa ya kaskazini ni mwamba ambao hauzidi futi 200 juu ya usawa wa bahari. Mwamba huu umeambatana na ardhi yenye rutuba inayoruhusu kilimo cha kila mwaka. Kwa upande wa pwani ya mashariki kuna miamba inayozuia shughuli za kilimo.

Kisiwa cha Mafia ni sehemu ya kwanza kuanzishwa Hifadhi ya Bahari Tanzania ilyoanzishwa rasmi mwaka 1995. Eneo la hifadhi limechukua sehemu zote ya kusini ya kisiwa na baadhi tu ya maeneo ya kasakazini.
(angalia ramani www.effectivempa.noaa.gov/images/maps/Mafia_map_1g.jpg

Maeneo ya Hifadhi ya Bahari yaliyodhibitiwa yamekusanya mazingira bahari yaliyomuhimu sana duniani ambapo yamejumuisha: mikoko, mwani, mafumbawe, majangwa, na misitu ya pwani. Ingawaje pamekuwa na mwamko katika kutambua umuhimu wa Hifadhi ya Bahari lakini vilevile kumekuwepo na matatizo kama vile uvuvi wa kupindukia (haswa kutokana na wavuvi ya kigeni na uvuvi wa baruti).

Utafiti wa kwanza wa eneo hilo ulifanywa na Frontier Organisation: www.frontierprojects.ac.uk, , ambao huchapisha matoleo mabalimbali ya ripoti za ekolojia ya Kisiwa cha Mafia (angalia Horrill and Ngoille 1992). Ingawaje Frontier wamesitisha kazi zao Kisiwani Mafia, bado kuna vyuo kadhaa vya kigeni vinavyowatuma wanafunzi wao kama sehemu ya kozi zao za ekolojia ya pwani. Mafano: www.sit.edu/studyabroad/africa/tanzcoast_pom.html

Uamuzi wa kuundwa kwa Hifadhi ya Bahari ulichukuliwa na serikali ya Tanzania na kwa sasa MIMP iko chini ya kitengo cha Hifadhi ya Bahari na Udhibiti (www.marineparktz.com). MIMP inafadhiliwa na World Wildlife Fund (WWF) na habari zaidi zinapataikana katika www.peopleandplanet.net/pdoc/php?id=2178 na katika saiti ya WWF www.panda.org . Msaada mkubwa umetolewa na Idara ya Masuala ya Kimaendeleo ya Kimataifa ya huko Uingereza (Department for International Development - angalia (www.dfid.gov.uk) na vilevile kutoka shirika la msaada la Norway (http://www.norad.no) ana kiasi kidogo kutoka katika makampuni binafsi (m.f. www.fmc.com/Corporate/V2/NewsDetail/0,1597,1694.html)

Ferry furling its sails at sunsetHabari zaidi za hifadhi hii zinapatikana katika mitandao inayoichukulia hifadhi hii ya Mafia kama mfano wa kuigwa: http://effectivempa/noaa.gov/sites/mafia.html na katika mtandao ya UNESCO: ioc.unesco.org/oceanportal/detail.php?id=1847

Mbali ya kuzungumzia masuala ya ikolojia, tovuti mbalimbali zimejishughulisha pia na kuangalia kwa kiasi gani muundo wa Hifadhi ya Bahari umeathiri mifumo ya kijamii. Makala ya Peter Denton yameangalia mfumo wa utoaji mikopo wa MIMP: www.peopleandplanet.net/pdoc.php?id=2178 wakati stashahada ya Esther Japhet Mullilya iitwayo Socio-economic impacts of marine protected areas: the case of Mafia Island Marine Park in Tanzania inayopatikana www.nfh.uit.no/dok/IFM/abstracts/1999/esther.html

Wanataaluma mbalimbali wamejihusisha na tafiti zihusuzo namna ya uundwaji na utendaji wa Hifadhi ya Bahari Kisiwani Mafia. Kazi ya mwanaanthropolojia Christine Walley ni ya muhimu, pamoja na habari zilizomo katika kitabu chake cha hivi karibuni kiitwacho Rough Waters: Nature and Development in an East African Marine Park inayopatikana katika mtandao wa mchapishaji wake: pup.princeton.edu/titles/7775.html

Makala yahusuyo athari za Hifadhi Mazingira Bahari inapatikana katika makala yake Chris Walley, 'Best intentions: the story of Tanzania's people's park' (www.bostonreview.net/BR29.6/walley.html). Makala ya Arielle Levine yahusuyo 'Global Partnerships in Tanzania's Marine Resource Management: NGOs, the private sector, and local communities' yanautizama mradi wa MIMP kama sehemu ya utatuzi wa mradi unaosaidia kuhifadhi mzaningira bahari: http://dlc/dlib.indiana.edu/archives/00000852/00levinea030602.pdf

Marejeo ya msingi na ya ziada.

  • Board of Trustees, Maine Parks and Reserves, Tanzania, 2000. Mafia Island Marine Park General Management Plan. Ministry of Natural Resources and Tourism, United Republic of Tanzania (a Swahili version of this is also available)

  • Horrill, Jc and MAK Ngoile, 1992. Mafia Island Project Report number 2 (vol. 1 text, vol. 2 appendices) The Society for Environmental Exploration and the University of Dar es Salaam.

  • Mayers, C.J., MAK Ngoile, J.C. Horrill, P. Nnyiti, C.K. Runisha, T.R. Young, 1992. The Proposed Mafia Island Marine Park: Discussion Paper, Tanzania Ministry of Tourism, Natural Resources and Environment.

  • Walley, Christine, 2004. Rough Waters: Nature and Development in an African Marine Park. Princeton and Oxford: Princeton University Press.