MAFIA ISLAND TANZANIA image branding - people of Mafia Island

Nyumbani

Akiolojia na Historia

Idadi ya watu na sensa

Ikiolojia (pamoja na Hifadhi ya Bahari)

Uchumi

Utalii

Afya na miradi ya afya

Vyama hiari

Habari mbalimbali za Kisiwa cha Mafia

Picha za Mafia

English Home

Akioloji na Historia

Kisiwa cha Mafia na vinginevyo vilivyosambaa mwambao wa Bahari ya Hindi vina historia ndefu ya kuvutia. Mwambao wa pwani ni sehemu ya pwani ya Bahari ya Hindi na watu wa maeneo haya wamekuwa wafanyabiashara na mabaharia kwa karne nyingi. Imekuwa ni ya aina yake kwani kumbukumbu zake zimeandikwa tangu miaka elfu mbili iliyopita katika maandishi ya mwanzo ya kigiriki ya Periplus of the Erythraen Sea, ambayo yameandikwa mnamo A.D. 110. Taarifa zilizoandikwa baada ya hapo hadi kipindi cha ujio wa Wareno katika pwani katika karne ya kumi na tano ziliandikwa na wanajiografia wa Kiaarabu.

Mwishoni mwa Milenia ya kwanza (A.D), tayari kulikuwa kumeanzishwa miji ya kiislamu iliyojihusha na biashara, ilikuwa imeshaimarika katika visiwa vya Unguja na Pemba. Katika kipindi cha karne ya kumi na tatu, makao makuu yalikuwa Kilwa Kisiwani, kisiwa kidogo kilichopo maili 80 kusini mwa Kisiwa cha Mafia. Kilwa ilipata umashuhuri kwa kuwa ni njia kuu ya biashara ya dhahabu kutokea Sofala (kwa sasa ni sehemu ya Msumbiji).

Maandishi ya mwanzo yanayohusiana na habari za pwani yapo katika Kilwa Chronicle, ambapo yamesalia makala yake mawili, moja kwa kiarabu na jengine kwa kireno. Katika kitabu hiki insemekana kuwa mji wa Kilwa ulianzishwa na watoto wa sultani kutokea Shirazi, Ghuba ya Uajemi, ambao walihamia katika karne ya kumi (A.D). Kilwa Chronicle iliendelea kurekodi kwamba baadhi ya watoto Sultani wa kwanza wa Kilwa waliweka makazi yao katika upande wa kusini-magharibi ya Kisiwa cha Mafia; sehemu ijulikanayo kama Kisimani Mafia.

Kipindi cha kati ya karne ya kumi na mbili na kumi na tano kilikuwa ni kilele cha ustaarabu wa miji ya kiislamu: watawala wao na wafanyabiashara walijenga misikiti mikubwa, makaburi na majumba, sarafu zenye chapa, na vilevile waliagizia vyombo vya kauri kutokea sehemu mbalimbali duniani ikiwepo China. Miji hii ilikuwa na Waafrika na wafanyabiashara kutokea sehemu nyenginezo za Bahari ya Hindi, hususani Ghuba ya Uajemi.

Wareno walifika pwani ya Afrika mnamo mwaka 1498 na wakasalia humo kwa miaka miambili. Walimiliki machimbo ya dhahabu ya Sofala na kusababisha kuanguka kwa umaarufu wa Kilwa. Hatahivyo waliacha athari chache tu kama vile ngome kubwa za Kilwa na Mombasa na baadhi ya misamiati ya kireno kama vile meza na almari.

Wareno waling'olewa na waarabu wa Omani waliotawala pwani na pande za bara kuanzia mwanzoni mwa karne ya kumi na nane hadi mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Wakati huo Waingereza na Wajerumani walianza kutawala Kenya na Tanganyika. Wakati wa utawala wa Omani, mji muhimu kuliko wote ulikuwa Unguja. Makao makuu ya sultani katika kipindi hiki mahusiano baina ya bara na visiwani yaliimarika haswa kutokana na biashara ya pembe na watumwa. Katika kipindi hiki kulikuwa na usemi kuwa ' ipigwapo zumari Unguja watu hucheza hadi Maziwani'. Kupanuka kwa biashara kuliendana sambamba na kuenea kwa lugha ya Kiswahili na uandishi hadi bara ndani. Kwa kipindi chote hiki, Kisiwa cha Mafia haikuwa na uhuru wake. Zama za kati kilitawaliwa na Kilwa, na baadaye Unguja (ramani ionyeshayo jinsi Kilwa na Kisiwa cha Mafia ilvyosehemu ya Unguja www.zum.de/whkmla/region/eastafrica/tangpre115.html). Ni katika kipindi hiki ndipo Waarabu wengi wenye asili ya kiOmani walihamia Kisiwa cha Mafia kusini na kuanzisha mashamba makubwa ya minazi wakitumia watumwa walioletwa kutoka bara. Wenyeji wa Kisiwa cha Mafia waliojiita Wambwera au Washirazi walijisogeza sehemu za kaskazini ambako ardhi yake si nzuri kwa kilimo cha minazi lakini ilikubali kilimo cha mazao ya kujikimu.

Mnamo mwaka 1890, Kisiwa cha Mafia, ambacho hadi kipindi hicho kilikuwa chini ya himaya ya Sultani wa Unguja, kilihamia chini ya utawala ya Kijerumani mara baada ya 'kuuzwa' na Waingereza ili wao Waingereza wachukuwe ukanda wa nchi uliojulikana kama Barabara ya Stephenson kati ya Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika. Kilimo cha minazi kiliongezeka. Wajerumani wenyewe walikuwa na mashamba makubwa na hivyo wakawalazimisha kila wanaume watu wazima sharti wawe na minazi isiyopungua minazi hamsini kwa ajili ya mbata (kwa matumizi mbalimbali) na kuwafanya wawe na fedha za kulipa kodi. Walikifanya kisiwa kidogo cha Chole kilichopo kusini magharibi ya kisiwa kikuu cha Kisiwa cha Mafia kama makao yao makuu.

Majeshi ya Kiingereza walishika madaraka ya Kisiwa cha Mafia wakati wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918), matokeo yake kikawa chini ya usimamizi na udhamini wa Umoja wa Mataifa (League of Nations) wa nchi ya Tanganyika. Nchi hiyo ilijipatia uhuru wake mnamo mwaka 1961 na ndipo mwaka 1964 ilipoungana na Unguja kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wazungu walianza kumiliki mashamba ya minazi yaliyopo kusini zaidi katika kipindi cha utawala wa kiingereza. Na makao ya makuu ya wilaya yakahamishiwa Kilindoni. Umiliki wa Waarabu wa mashamba ya minazi ulififia mara baada ya kampeni ya kuachiwa huru kwa watumwa mnamo mwaka 1922. Kwa uthibitisho wa vitambulisho walivyokuwa wakipewa watumwa kisiwani Chole na wajerumani hapo mwaka 1911 angalia
http://worldhistoryconnected.press.uiuc.edu/1.1/gilbert.htm

Ni katika kipindi cha utawala wa Wazungu, tulishuhudiwa kujitenga kwa Kisiwa cha Mafia kama sehemu ya pwani (chini ya utawala wa Kilwa na Unguja) na kujiegemeza kiuchumi na kisiasa na bara, na ni katika kipindi hiki vilevile tunashuhudiwa kujitenga na kudidimia kwa Dar es Salaam.

Kumbukumbu za historia ya Kisiwa cha Mafia si nyingi au ndefu. Ziara aliyoifanya mwanajiografia Wakijerumani aitwaye Oscar Baumann katika Kisiwa cha Mafia mwishoni mwa karne ya kumi na tisa ilipelekea kupatikana kwa kazi ndefu inayoelezea kisiwa hicho kwa lugha ya Kijerumani (Baumann 1986) ambayo ilitafsiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa katika jarida la Tanganyika Notes and Records (Freeman-Grenville 1957). Mbali ya machapicho hayo, historia ya Kisiwa cha Mafia inapatikana kwa kukusanya hapa na pale matoleo mbalimbali yahusuyo historia na akiolojia ya Kilwa zaidi kuliko Kisiwa cha Mafia. Orodha ya marejeo ipo mwishoni mwa sehemu hii.

Katika kipindi cha miaka ya 90 mwanaanthropolojia, Christine Walley alifanya utafiti uliohusina na kisiwa cha Chole na kukusanya kiasi kikubwa cha maelezo ya kihistoria (Walley 2004, Sura ya 2; Iles na Walley nd). Aligawa historia hiyo katika sehemu tatu:

  • Miji ya kipindi cha kati ya Kua na Kisimani Mafia
  • ipindi cha utawala wa Omani cha karne ya kati na mwishoni mwa karne ya kumi na tisa. Kipindi ambacho utumwa wa mashamba ulitapakaa na Chole ilipokuwa makao ya Kisiwa cha Mafia
  • ipindi cha utawala wa Wazungu mwishoni mwa karne ya kumi na tisa hadi katikati ya karne ya ishirini
Magofu ya kale katika Kisiwa cha Mafia yapo Kisimani Mafia karibu na Kilindoni. Mengi yao yamefunikwa na bahari lakini kwa mujibu wa mwanaakiolojia Neville Chittick, aliyefanya machimbuzi yake katika mwaka 1950 aliundua kuwa ukanda wa mwanzo wenye mabaki ya misikiti ilikadiriwa kuwepo katika karne ya kumi na kumi na moja. Mwanakiolojia mwengine wa kiingereza aliyafanya uchunguzi wake sehemu za kisiwa cha Juani mnamo mwaka 1950 aligundua sarafu zilizotumika katika karne ya kumi na tatu na kumi na tano (Freeman-Grenville 1957). Baadhi ya wanaakiolojia walichukulia Kua ilijengwa kabla ya hapo, bali wengine walihesabia tarehe ya mbele zaidi. Kulikuwa na hekaya inayoelezea uadui uliokuwapo baina ya Kua na Juani kama ulivyojitokeza katika kazi za ushairi na nathari zilizokusanywa na Mjerumani Carl Velten (1907) na tafsiri yake ya Kiingereza iliyojitokeza katika Swahili Coast magazine toleo la 5 lipatikanalo kupitia.

Taarifa ya msaidizi wa uchunguzi wa Walley pia amesimulia kisa hicho (Walley 2004, chapter 2).

Uchunguzi wa hivi karibuni wa kiakiolojia katika kisiwa cha Mafia uliofanywa na mwanaakiolojia wa Kitanzania aitwaye Felix Chami ulionyesha kuwa Waswahili walikuwepo na walikuwa na mashirikiano baina yao kwa kipindi kirefu nyuma. Ni hivi karibuni tu aligundua pango katika kisiwa cha Juani. Kwa kazi zake zaidi angalia.

www/arkeologi.uu.sae/afr/symposium/abstracts/chami/htm

Marejeo